Exodus 20:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo na mbuzi, na ng’ombe wako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ng'ombe zako. Po pote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ng’ombe zako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unijengee kwa udongo pa kunitambikia, upate pa kunitolea ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukruni za kondoo wako na za ng'ombe wako! Napo po pote, nitakapokukumbusha Jina langu, nitakuja kwako, nikubariki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng’ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mutanijengea mazabahu ya udongo. Juu yake mutanitolea kondoo wenu na ngombe wenu kama sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Pahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, pale pale mimi mwenyewe nitawafikia na kuwabariki.