Exodus 20:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanaonichukia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usivisujudie au kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usivitambikie, wala usivitumikie! Kwani mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; manza za baba nitazipatilizia wana, nikifikishe kizazi cha tatu na cha nne, kwao wanichukiao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiiname mbele yao wala kuvitumikia, kwa sababu mimi Yawe, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Ninawaazibu wana kwa ajili ya maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha ine cha wale wanaonichukia.