Exodus 21:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wanaume wakipigana na kumwumiza mwanamke mjamzito, hata mimba yake ikaharibika bila madhara mengine zaidi, yule aliyemwumiza atatozwa faini kama atakavyodai mumewe mwanamke huyo na kama mahakimu watakavyoamua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watu wawili wakipigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wanaume wakipigana na kumwumiza mwanamke mjamzito, hata mimba yake ikaharibika bila madhara mengine zaidi, yule aliyemwumiza atatozwa faini kama atakavyodai mumewe mwanamke huyo na kama mahakimu watakavyoamua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamwumiza mwanamke mja mzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wanaume wakipigana, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wanaume wakipigana na kumwumiza mwanamke mjamzito, hata mimba yake ikaharibika bila madhara mengine zaidi, yule aliyemwumiza atatozwa faini kama atakavyodai mumewe mwanamke huyo na kama mahakimu watakavyoamua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wakigombana, tena hapo wakipiga mwanamke mwenye mimba, nayo mimba yake ikiharibika pasipo kumtia ugonjwa, sharti atozwe fedha, kama mumewe yule mwanamke atakavyomtakia; hana budi kuzitoa zizo hizo, waamuzi watakazomwagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanaume wakipigana na kumwumiza mwanamuke mwenye mimba, hata mimba yake ikaharibika bila hasara ingine zaidi, yule aliyemwumiza atalipa feza kadiri mume wa mwanamuke yule atakavyodai na kama vile waamuzi watakavyoamua.