Exodus 21:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama ng'ombe huyo amezoea kupiga watu pembe, na mwenyewe akaonywa lakini hakumfunga, kama ng'ombe huyo akiua mtu lazima apigwe mawe, na mwenyewe lazima auawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama ng'ombe huyo amezoea kupiga watu pembe, na mwenyewe akaonywa lakini hakumfunga, kama ng'ombe huyo akiua mtu lazima apigwe mawe, na mwenyewe lazima auawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamwua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo mwanzo, naye mwenyewe ameoneshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mwanamume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama ng'ombe huyo amezoea kupiga watu pembe, na mwenyewe akaonywa lakini hakumfunga, kama ng'ombe huyo akiua mtu lazima apigwe mawe, na mwenyewe lazima auawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama huyo ng'ombe alikuwa akikumba watu tangu siku nyingi, naye bwana wake alikuwa ameonywa, lakini hakumwangalia huyo ng'ombe, naye akiua mwanamume au mwanamke, basi, huyo ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe, naye bwana wake hana budi kuuawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama ngombe yule amezoea kupiga watu pembe, na mwenye ngombe akaonywa lakini hakumufunga, kama ngombe yule akiua mume au muke, ngombe yule atapigwa mawe, na mwenye ngombe vilevile atauawa.