Exodus 21:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama bwana wake alimwoza mke, akamzalia watoto wa kike au wa kiume, basi, huyo mwanamke na watoto wake watakuwa mali ya huyo bwana wake, na huyo mtumwa ataondoka peke yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake, na huyo mwanaume ataondoka peke yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama bwana wake alimwoza mke, akamzalia watoto wa kike au wa kiume, basi, huyo mwanamke na watoto wake watakuwa mali ya huyo bwana wake, na huyo mtumwa ataondoka peke yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikiwa ni bwana wake aliyemwoza huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama bwana wake alimwoza mke, akamzalia watoto wa kike au wa kiume, basi, huyo mwanamke na watoto wake watakuwa mali ya huyo bwana wake, na huyo mtumwa ataondoka peke yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama bwana wake alimpa mwanamke, naye akazaa wana wa kiume na wa kike, yule mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wao, naye mume atatoka utumwani peke yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama bwana wake alimwoea muke, akamuzalia watoto wanawake au wanaume, basi, yule mwanamuke na watoto wake watakuwa mali ya yule bwana wake na yule mutumwa ataondoka peke yake.