Exodus 21:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa huyo bwana wake alimnunua awe mmoja wa wake zake, kisha asipendezwe naye, huyo bwana atamwacha baba yake huyo mtumwa amkomboe. Huyo bwana hana haki ya kumwuza kwa watu wa mataifa mengine, kwa kuwa atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa huyo bwana wake alimnunua awe mmoja wa wake zake, kisha asipendezwe naye, huyo bwana atamwacha baba yake huyo mtumwa amkomboe. Huyo bwana hana haki ya kumwuza kwa watu wa mataifa mengine, kwa kuwa atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumwuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikiwa bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa huyo bwana wake alimnunua awe mmoja wa wake zake, kisha asipendezwe naye, huyo bwana atamwacha baba yake huyo mtumwa amkomboe. Huyo bwana hana haki ya kumwuza kwa watu wa mataifa mengine, kwa kuwa atakuwa amekosa uaminifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiwa mbaya machoni pa bwana wake aliyemtaka wa kulala naye, na amtoe, akombolewe; lakini hana ruhusa ya kumwuza kwa watu wa kabila geni, kwani ni yeye aliyemdanganya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa yule bwana wake alimununua akuwe mumoja wa wake zake, kisha asipendezwe naye, yule bwana ataacha baba ya yule mujakazi amukomboe. Yule bwana hana haki ya kumwuzisha kwa watu wa mataifa mengine, akiwa amemudanganya.