Exodus 22:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kiapo mbele ya Mwenyezi-Mungu kitaamua kati yao, kuonesha kwamba huyo aliyekabidhiwa hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake. Mwenye mnyama huyo atakubali hicho kiapo, na huyo mwenzake hatalipa malipo yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa mbele za Mwenyezi Mungu, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
patakuwa na kiapo cha Bwana katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kiapo mbele ya Mwenyezi-Mungu kitaamua kati yao, kuonesha kwamba huyo aliyekabidhiwa hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake. Mwenye mnyama huyo atakubali hicho kiapo, na huyo mwenzake hatalipa malipo yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za BWANA, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za bwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
patakuwa na kiapo cha BWANA katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kiapo mbele ya Mwenyezi-Mungu kitaamua kati yao, kuonesha kwamba huyo aliyekabidhiwa hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake. Mwenye mnyama huyo atakubali hicho kiapo, na huyo mwenzake hatalipa malipo yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mwenyewe na amwapishe mwenzake, amtaje Bwana kwamba hakuchukua mali ya mwenzake kwa mkono wake, kisha yule, mwenzake hana budi kumwitikia, asilipe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
patakuwa na kiapo cha BWANA katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama aliibiwa kwake, anapaswa kumulipa mwenye naye.