Exodus 22:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama huyo mnyama aliraruliwa na wanyama wa porini, huyo mtu aliyekuwa amekabidhiwa lazima amlete kama ushahidi. Hatalipa malipo yoyote kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama wa porini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa mnyama aliyeraruliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwamba aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama huyo mnyama aliraruliwa na wanyama wa porini, huyo mtu aliyekuwa amekabidhiwa lazima amlete kama ushahidi. Hatalipa malipo yoyote kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama wa porini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama huyo mnyama aliraruliwa na wanyama wa porini, huyo mtu aliyekuwa amekabidhiwa lazima amlete kama ushahidi. Hatalipa malipo yoyote kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama wa porini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiraruliwa na nyama, sharti amlete huyo nyama aliyeraruliwa kuwa ushahidi; basi, hivyo hatamlipa aliyeraruliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwamba aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akiazima nyama kwa mwenzake, kisha nyama yule akaumia au akakufa wakati mwenye naye hayuko, aliyeazima nyama yule anapaswa kumulipa kwa ukamilifu.