Exodus 22:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama mwenyewe alikuwako, basi aliyemwazima hatalipa chochote. Kama alikuwa ni mnyama aliyekodishwa, mwenyewe ataikubali tu bei ya kukodisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mwenye mnyama akiwa bado ako na mnyama wake, aliyeazima hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama aliyeajiriwa, alikwenda kwa ajili ya ujira wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama mwenyewe alikuwako, basi aliyemwazima hatalipa chochote. Kama alikuwa ni mnyama aliyekodishwa, mwenyewe ataikubali tu bei ya kukodisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama wa kukodisha ni gharama ya kukodisha tu atakayepewa mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama mwenyewe alikuwako, basi aliyemwazima hatalipa chochote. Kama alikuwa ni mnyama aliyekodishwa, mwenyewe ataikubali tu bei ya kukodisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama bwana wake yuko hapo, halipi; kama alimkodisha huyo nyama, malipo yamo katika hizo fedha za kukodisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama aliyeajiriwa, alikwenda kwa ajili ya ujira wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akimutongoza binti ambaye hajachumbiwa, akilala naye, hakika atalipa mali na kumwoa binti yule.