Exodus 22:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu akiwalisha wanyama wake katika shamba la mizabibu au kumwachia mnyama wake kula katika shamba la mtu mwingine, atalipa hasara hiyo kwa mazao bora ya shamba lake mwenyewe au shamba lake la mizabibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia walishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu akilisha katika shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu akiwalisha wanyama wake katika shamba la mizabibu au kumwachia mnyama wake kula katika shamba la mtu mwingine, atalipa hasara hiyo kwa mazao bora ya shamba lake mwenyewe au shamba lake la mizabibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka katika shamba lake la mizabibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu akilisha mifugo katika shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu akiwalisha wanyama wake katika shamba la mizabibu au kumwachia mnyama wake kula katika shamba la mtu mwingine, atalipa hasara hiyo kwa mazao bora ya shamba lake mwenyewe au shamba lake la mizabibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akilisha shamba au mizabibu, akiliacha kundi lake, lijiendee kulisha shambani kwa mwingine, sharti amlipe na kuyatoa mazao ya shamba lake yeye na ya mizabibu yake yeye yaliyo mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu akilisha katika shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akiwasha moto nao ukichoma miti ya miiba na kusambaa mpaka kuteketeza miganda ya ngano au ngano ya mutu mwingine ambayo bado haijavunwa au shamba lote likiteketea, aliyewasha moto ule anapaswa kulipa hasara ile yote.