Exodus 22:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu akiwasha moto nao ukachoma miti ya miiba na kusambaa hadi kuteketeza miganda ya nafaka, au nafaka ya mtu mwingine ambayo bado haijavunwa, au shamba lote likateketea, aliyewasha moto huo lazima alipe hasara hiyo yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu akiwasha moto nao ukachoma miti ya miiba na kusambaa hadi kuteketeza miganda ya nafaka, au nafaka ya mtu mwingine ambayo bado haijavunwa, au shamba lote likateketea, aliyewasha moto huo lazima alipe hasara hiyo yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu akiwasha moto nao ukachoma miti ya miiba na kusambaa hadi kuteketeza miganda ya nafaka, au nafaka ya mtu mwingine ambayo bado haijavunwa, au shamba lote likateketea, aliyewasha moto huo lazima alipe hasara hiyo yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Moto ukitoka kwenye kuchoma miiba, ukala miganda iliyokwisha kufungwa au mabua yenye ngano au shamba lo lote, basi, mwenye kuuwasha huo moto sharti ayalipe yaliyoharibika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akimwachia mwenzake feza au mali nyingine amutunzie, kisha ikaibiwa ndani ya nyumba yake, mwizi akipatikana anapaswa kulipa bei yake mara mbili.