Exodus 22:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atakaribia mbele za Mungu ili kuthibitisha kwamba hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwivi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atakaribia mbele za Mungu ili kuthibitisha kwamba hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwizi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atakaribia mbele za Mungu ili kuthibitisha kwamba hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwizi asipoonekana, mwenye nyumba na apelekwe kwa Mungu, waone, kama siye mwenyewe aliyevichukua vyombo vya mwenzake kwa mkono wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwivi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukitokea ubishi juu ya ngombe, au punda, au kondoo, au nguo, au kitu chochote kilichopotea ambacho kila mumoja anadai kwamba ni chake, wale wanaobishana wataletwa mbele ya Mungu. Yule ambaye Mungu ataamua kwamba amekosa, atamulipa mwenzake mara mbili.