Exodus 23:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye akiwa ameanguka chini ya mzigo wake, na wewe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukimwona punda wa mchukivu wako, ya kuwa ameanguka kwa kulemewa na mzigo wake, usiwaache peke yao, ila yaache mambo yako, usaidiane navyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukimwona punda wa mutu anayekuchukia ameanguka na muzigo wake, umusaidie mutu yule kumusimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.