Exodus 24:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukatua juu ya mlima Sinai na wingu likaufunika mlima kwa muda wa siku sita. Siku ya saba Mungu akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Mwenyezi Mungu akamwita Musa kutoka kati ya lile wingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huo utukufu wa Bwana ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukatua juu ya mlima Sinai na wingu likaufunika mlima kwa muda wa siku sita. Siku ya saba Mungu akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao utukufu wa BWANA ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba BWANA akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao utukufu wa bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba bwana akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukatua juu ya mlima Sinai na wingu likaufunika mlima kwa muda wa siku sita. Siku ya saba Mungu akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao utukufu wa Bwana ukaja kukaa juu ya mlima wa sinai, nalo wingu likaufunika siku sita. Siku ya saba akamwita Mose toka winguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utukufu wa Yawe ukatua juu ya mulima Sinai na wingu likafunika mulima kwa muda wa siku sita. Siku ya saba Mungu akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu.