Exodus 24:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa akaandika kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose akaandika kila kitu BWANA alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa akaandika kila kitu bwana alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akayaandika maneno yote ya Bwana, akajidamka asubuhi, napo hapo chini penye huo mlima akajenga pa kutambikia, akapasimamishia nguzo kumi na mbili kwa hesabu ya mashina kumi na mawili ya Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akaandika maagizo yote ambayo Yawe alimupa. Kisha akaamuka asubui mapema, akajenga mazabahu chini ya mulima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na hesabu ya makabila kumi na mbili ya Israeli.