Exodus 25:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Utatengeneza kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake na ufito wa hicho kinara vitakuwa kitu kimoja, kadhalika na vikombe vyake, matumba yake na maua yake, vyote vitafuliwa kwa kipande kimoja tu cha dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Utatengeneza kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake na ufito wa hicho kinara vitakuwa kitu kimoja, kadhalika na vikombe vyake, matumba yake na maua yake, vyote vitafuliwa kwa kipande kimoja tu cha dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi nacho kiwe cha kazi ya kufua, tako lake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake, vitakuwa vya kitu kimoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Utatengeneza kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake na ufito wa hicho kinara vitakuwa kitu kimoja, kadhalika na vikombe vyake, matumba yake na maua yake, vyote vitafuliwa kwa kipande kimoja tu cha dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena utengeneze kinara cha dhahabu tupu! Hiki kinara na kitengenezwe kwa kufuafua dhahabu, ipate kutoka shina lake na mti wake, navyo vikombe vyake na vifundo vyake na maua yake, vyote pia viwe vimetoka katika dhahabu iyo hiyo moja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatengeneza kinara cha taa kwa zahabu safi. Tako lake na muti wa kile kinara vitakuwa kitu kimoja, vilevile na vikombe vyake. Mafundo yake na maua yake, vyote vitafuliwa kwa kipande kimoja tu cha zahabu.