Exodus 25:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kila tawi kutakuwa na vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi, kila kimoja na tumba lake na ua lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kila tawi kutakuwa na vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi, kila kimoja na tumba lake na ua lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua yawe katika tawi moja, matovu matatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyoanzia kwenye kinara cha taa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika kila tawi kutakuwa na vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi, kila kimoja na tumba lake na ua lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vikombe vitatu vinavyofanana na maua ya mlozi viwe katika kila tawi moja, yaani vifundo pamoja na maua yao. Vivyo hivyo katika matawi yote sita yanayotoka katika mti wa kinara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kila tawi kutakuwa vikombe vitatu mufano wa maua ya lozi, kila kimoja na kifundo chake na ua lake.