Exodus 26:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo kutakuwa na mbao nane pamoja na vikalio vyake kumi na sita vya fedha: Vikalio viwili chini ya kila mbao na vikalio viwili chini ya ubao mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo kutakuwa mihimili nane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbao zitakuwa ni nane, na matako yake ya fedha, matako kumi na sita; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao wa pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo kutakuwa na mbao nane pamoja na vikalio vyake kumi na sita vya fedha: vikalio viwili chini ya kila mbao na vikalio viwili chini ya ubao mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbao zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha, vitako kumi na sita; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo kutakuwa na mbao nane pamoja na vikalio vyake kumi na sita vya fedha: Vikalio viwili chini ya kila mbao na vikalio viwili chini ya ubao mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo zote pamoja zitakuwa mbao nane, navyo viguu vya fedha vitakuwa kumi na sita, viguu viwili chini ya kila ubao mmoja, viwe viguu viwili chini ya kila ubao mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbao zitakuwa ni nane, na matako yake ya fedha, matako kumi na sita; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao wa pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo kutakuwa mbao nane pamoja na vikalio vyake kumi na sita vya feza: vikalio viwili chini ya kila mbao na vikalio viwili chini ya ubao mwingine.