Exodus 26:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Utatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa. Pazia hilo utalitarizi kwa ustadi kwa viumbe wenye mabawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Utatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa. Pazia hilo utalitarizi kwa ustadi kwa viumbe wenye mabawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atarizi makerubi kwenye hayo mapazia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Utatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa. Pazia hilo utalitarizi kwa ustadi kwa viumbe wenye mabawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena utengeneze pazia lililoshonwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu. Fundi wa kufuma na alitengeneze kuwa lenye mifano ya Makerubi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya samawi, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa. Juu ya pazia lile utachora kwa ufundi sanamu za makerubi.