Exodus 26:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ning'iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili pazia ulitungike chini ya hivyo vifungo, kisha uliingize Sanduku la Ushahidi mbele yake pazia, hilo pazia liwatengee Patakatifu na Patakatifu Penyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatundika pazia lile kwenye vifungio, kisha ulete lile Sanduku la Agano mule ndani, nyuma ya pazia lile. Pazia lile litatenga Pahali Patakatifu na Pahali Patakatifu Sana.