Exodus 26:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ile meza ya mjohoro utaiweka upande wa nje wa pazia hilo, na kile kinara cha taa utakiweka upande wa kusini wa hema, mkabala wa meza. Meza hiyo itakuwa upande wa kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa maskani ya Mungu, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa maskani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ile meza ya mjohoro utaiweka upande wa nje wa pazia hilo, na kile kinara cha taa utakiweka upande wa kusini wa hema, mkabala wa meza. Meza hiyo itakuwa upande wa kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ile meza ya mjohoro utaiweka upande wa nje wa pazia hilo, na kile kinara cha taa utakiweka upande wa kusini wa hema, mkabala wa meza. Meza hiyo itakuwa upande wa kaskazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo ile meza iweke upande wa huku wa pazia, na kinara kile kiweke kuilekea meza upande wa kusini wa kao, lakini meza uiweke upande wa kaskazini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ile meza ya mujohoro utaiweka upande wa inje wa pazia lile, na kile kinara cha taa utakiweka upande wa kusini wa hema, kikielekeana na meza. Meza ile itakuwa upande wa kaskazini.