Exodus 26:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa ajili ya mlango wa hema utatengeneza pazia zito kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa ajili ya mlango wa hema utatengeneza pazia zito kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa ajili ya lango la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, ambayo ni kazi ya mtarizi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa ajili ya mlango wa hema utatengeneza pazia zito kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha hapo pa kuingia hemani uweke guo kubwa lililotengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, lifumwe nao wanaojua kweli kufuma kwa nyuzi za rangi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ajili ya mulango wa hema utatengeneza pazia zito kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kuchorwa vizuri.