Exodus 26:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utashonea vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, hali kadhalika utashonea vitanzi mwishoni mwa pindo la nje la kipande kingine cha pazia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha utafanya tanzi za rangi ya samawi upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utashonea vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, hali kadhalika utashonea vitanzi mwishoni mwa pindo la nje la kipande kingine cha pazia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye ukingo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, pia kipande cha mwisho cha pazia la pili ufanye vivyo hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha utafanya tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa lile pazia lililo katika fungu la pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utashonea vitanzi vya buluu upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, hali kadhalika utashonea vitanzi mwishoni mwa pindo la nje la kipande kingine cha pazia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha ushone vitanzi vya nguo nyeusi za kifalme penye upindo wa nje wa kila pazia moja hapo, litakapoungwa na jingine; vivyo hivyo uvitie napo penye upindo wa nje wwa kila pazia la pili hapo, litakapoungwa nalo la kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha utafanya tanzi za rangi ya samawi upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utashonea kamba za rangi ya samawi kwenye upindo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza. Vilevile utashonea kamba kwa mwisho wa pindo la inje la kipande kingine cha pazia.