Exodus 27:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake ni dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano na upana wake dhiraa tano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tengeneza meza ya kutambikia kwa mbao za migunga! Urefu wake uwe mikono mitano, nao upana wake uwe mikono mitano, hiyo meza iwe sawa pande zote nne, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mikono mitatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatengeneza mazabahu kwa mbao za mujohoro. Mazabahu ile itakuwa ya muraba, urefu wake metre mbili na sentimetre makumi mbili, na upana wake metre mbili na sentimetre makumi mbili. Urefu kwenda juu utakuwa metre moja na sentimetre makumi mbili.