Exodus 27:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na matako yake ishirini, matako yake yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini. Pia kutakuwa na kulabu za fedha na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nguzo zake ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba; vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na matako yake ishirini, matako yake yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nguo zile zitashikiliwa na nguzo makumi mbili za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini vifungio vya nguzo zile na kamba zake vitakuwa vya feza.