Exodus 27:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika upande wa kaskazini, urefu wa chandarua utakuwa mita 44, na nguzo zake 20 za shaba, lakini kulabu za nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni vivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia, na nguzo zake ishirini, na matako yake ishirini yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika upande wa kaskazini, urefu wa chandarua utakuwa mita 44, na nguzo zake 20 za shaba, lakini kulabu za nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upande wa kaskazini itakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia na nguzo zake ishirini, na vitako ishirini vya shaba, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika upande wa kaskazini, urefu wa chandarua utakuwa mita 44, na nguzo zake 20 za shaba, lakini kulabu za nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata upande wa kaskazini viwe vivyo hivyo: nguo ziwe zenye urefu wa mikono mia, nazo nguzo zao ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba, navyo vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni vivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia, na nguzo zake ishirini, na matako yake ishirini yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile upande wa kaskazini, urefu wa nguo utakuwa metre makumi ine na ine, na nguzo zake makumi mbili za shaba, lakini vifungio vya nguzo na kamba zake vitakuwa vya feza.