Exodus 27:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlango wenyewe wa ua utakuwa na pazia zito lenye urefu wa mita 9, lililotengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne zenye vikalio vinne.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na matako yake manne.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlango wenyewe wa ua utakuwa na pazia zito lenye urefu wa mita 9, lililotengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne zenye vikalio vinne.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kuhusu lango la kuingilia kwenye ua wa kukutania, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini, la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlango wenyewe wa ua utakuwa na pazia zito lenye urefu wa mita 9, lililotengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne zenye vikalio vinne.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo kati liwe lango la ua lenye pazia la mikono ishirini lililotengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, lifumwe nao wanaojua kufuma kwa nyuzi za rangi. Nguzo zake ziwe nne zenye miguu minne.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na matako yake manne.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulango wenyewe wa kiwanja utakuwa na pazia zito lenye urefu wa metre tisa, lililotengenezwa kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kuchorwa vizuri. Pazia lile litashikiliwa na nguzo ine zenye vikalio vine.