Exodus 27:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utaitengenezea vyombo vyake: Vyungu vya majivu, sepetu, na mabirika, na nyuma na visahani vya kuchukulia moto. Vyombo vyake vyote utavitengeneza kwa shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utaitengenezea vyombo vyake: vyungu vya majivu, sepetu, na mabirika, na nyuma na visahani vya kuchukulia moto. Vyombo vyake vyote utavitengeneza kwa shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, sepeto zake, mabakuli ya kunyunyizia, nyuma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utaitengenezea vyombo vyake: Vyungu vya majivu, sepetu, na mabirika, na nyuma na visahani vya kuchukulia moto. Vyombo vyake vyote utavitengeneza kwa shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyombo vyake vya kuondolea majivu na majembe yake na vyano vyake na nyuma zake na sinia zake, vyombo vyake vyote pia uvitengeneze kwa shaba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utaitengenezea vyombo vyake: vyungu vya kuwekea majivu, majembe, na mabeseni, na kanya na visahani vya kutwalia moto. Vyombo vyake vyote utavitengeneza kwa shaba.