Exodus 27:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Utatengeneza ua wa hema la mkutano. Upande wa kusini wa ua kutakuwa na vyandarua vilivyotengenezwa kwa kitani safi iliyosokotwa ambavyo vitakuwa na urefu wa mita 44 kwa upande mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Utatengeneza ua wa hema la mkutano. Upande wa kusini wa ua kutakuwa na vyandarua vilivyotengenezwa kwa kitani safi iliyosokotwa ambavyo vitakuwa na urefu wa mita 44 kwa upande mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na itakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Utatengeneza ua wa hema la mkutano. Upande wa kusini wa ua kutakuwa na vyandarua vilivyotengenezwa kwa kitani safi iliyosokotwa ambavyo vitakuwa na urefu wa mita 44 kwa upande mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha utengeneze ua wa hilo kao upande wa kusini ulio wa juani, nguo za huo ua zitengenezwe kwa bafta ngumu, nao urefu wa upande mmoja uwe mikono mia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatengeneza kiwanja cha hema la mukutano. Kwa upande wa kusini wa kiwanja kutakuwa nguo zilizotengenezwa kwa kitani safi iliyosokotwa ambazo zitakuwa na urefu wa metre makumi ine na ine kwa upande mumoja.