Exodus 28:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utayachora majina hayo juu ya hayo mawe kama vile sonara achoravyo mhuri, kisha uyatie nakshi na kuyaingiza katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utayachora majina hayo juu ya hayo mawe kama vile sonara achoravyo mhuri, kisha uyatie nakshi na kuyaingiza katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya hayo mawe mawili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uyatie hayo mawe katika vijalizo vya dhahabu
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kazi ya mtu mwenye kuchora mawe kama vile mihuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utayachora majina hayo juu ya hayo mawe kama vile sonara achoravyo mhuri, kisha uyatie nakshi na kuyaingiza katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kazi hii ya kuchora katika kito na uifanyishe mafundi wanaojua kuchora muhuri. Ndivyo, utakavyoyachora majina ya wanawe Isiraeli katika hivyo vito viwili; kisha uvizungushie vikingo vya dhahabu vya kuvishika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utayachora majina yale juu ya yale mawe kama vile muchoraji anavyochora muhuri, kisha uyaingize katika kingo za zahabu.