Exodus 28:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Utatengeneza kifuko cha kifuani cha kauli cha maamuzi; kitengenezwe kwa ustadi sawa kama kilivyotengenezwa kile kizibao: Kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tengeneza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kizibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Utatengeneza kifuko cha kifuani cha kauli cha maamuzi; kitengenezwe kwa ustadi sawa kama kilivyotengenezwa kile kizibao: kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha nyuzi za rangi ya dhahabu, buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Utatengeneza kifuko cha kifuani cha kauli cha maamuzi; kitengenezwe kwa ustadi sawa kama kilivyotengenezwa kile kizibao: Kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha kitengeneze kibati cha maamuzi cha kifuani, nacho kiwe kazi ya ufundi wa kweli. Ukitengeneze kuwa kazi nzuri kama ile ya kisibau, ukitumia kwa kukitengeneza dhahabu na nguo za kifame nyeusi na nyekundu na nguo za bafta ngumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatengeneza kifuko cha kifua cha maamuzi. Kitengenezwe kwa ufundi sawa vile kile kizibao kilivyotengenezwa: kwa zahabu, kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa.