Exodus 28:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, patakuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Kila moja litakuwa kama mhuri, ili kuwakilisha makabila yale kumi na mawili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, patakuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Kila moja litakuwa kama mhuri, ili kuwakilisha makabila yale kumi na mawili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Patakuwa na mawe kumi na mawili, moja kwa kila jina la wana wa Israeli, kila moja lichorwe kama muhuri likiwa na jina la moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, patakuwa na mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Kila moja litakuwa kama mhuri, ili kuwakilisha makabila yale kumi na mawili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hesabu ya majina ya wanawe Isiraeli viwe kumi na viwili vikiyafuata hayo majina yao, kila kimoja chao kipate jina lake moja katika hayo mashina kumi na mawili, likichorwa humo, kama kazi ya muhuri ilivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kutakuwa mawe kumi na mawili yaliyochorwa majina kumi na mawili ya wana wa Israeli. Kila moja litakuwa kama muhuri, kwa kusimamia makabila yale kumi na mawili.