Exodus 28:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha utatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzitia mbele katika ncha za chini za vipande vya kizibao, mahali kizibao kinapoungana na mkanda uliofumwa kwa ustadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uziunganishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega, upande wa mbele wa kile kizibau, karibu na pindo, juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kizibau.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe fanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha utatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzitia mbele katika ncha za chini za vipande vya kizibao, mahali kizibao kinapoungana na mkanda uliofumwa kwa ustadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tengeneza pete mbili zaidi za dhahabu na uzishikize mbele katika ncha za chini za vipande vya kisibau, mahali kinapoungana juu ya mshipi wa kiunoni wa kisibau.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe fanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha utatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzitia mbele katika ncha za chini za vipande vya kizibao, mahali kizibao kinapoungana na mkanda uliofumwa kwa ustadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha utengeneze tena pete mbili za dhahabu, uzitie katika vipande vile viwili vya mabegani vya kisibau chini upande wake wa mbele papo hapo, vile vipande vinapounganika, juu ya masombo ya kisibau.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe fanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utatengeneza pete zingine mbili za zahabu na kuzitia mbele katika incha za chini za vipande vya kizibao, pahali kizibao kinapoungana na mukaba uliofumwa kwa ufundi.