Exodus 28:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waagize mafundi wote ambao nimewapa maarifa wamtengenezee Aroni mavazi ili awekwe wakfu kwa ajili ya kazi ya ukuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Haruni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waagize mafundi wote ambao nimewapa maarifa wamtengenezee Aroni mavazi ili awekwe wakfu kwa ajili ya kazi ya ukuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Haruni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waagize mafundi wote ambao nimewapa maarifa wamtengenezee Aroni mavazi ili awekwe wakfu kwa ajili ya kazi ya ukuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe sema nao walio werevu wa kweli mioyoni mwao, niliowapa roho yenye werevu mwingi ulio wa kweli, wamtengenezee Haroni mavazi ya kumweulia, apate kuwa mtambikaji wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaagize wafundi wote ambao nimewapa maarifa wamutengenezee Haruni nguo kusudi atakaswe kwa ajili ya kazi ya ukuhani.