Exodus 28:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaninginie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Haruni kila mara aingiapo mbele za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo siku zote Haruni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya Waisraeli mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Bwana; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Bwana daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaning'inie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za BWANA. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Haruni kila mara aingiapo mbele za bwana. Kwa hiyo siku zote Haruni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele za BWANA; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele za BWANA daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaninginie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena utie katika kibati cha maamuzi cha kifuani Urimu na Tumimu (Mwanga na Kweli), ziwe juu ya moyo wake Haroni, atakapotokea usoni pa Bwana. Ndivyo, Haroni atakavyoyachukua maamuzi ya wana wa Isiraeli juu ya moyo wake usoni pa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya BWANA; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya BWANA daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya shauri yaninginie kwenye kifua cha Haruni kila mara anapokuja mbele yangu. Wakati ule anapaswa kila mara kuvaa kifuko kile, kusudi aweze kutambua mapenzi yangu juu ya Waisraeli.