Exodus 28:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni atavaa kanzu hiyo kutekeleza huduma yake ya ukuhani na sauti yake itasikika wakati anapoingia mahali patakatifu mbele yangu na wakati anapotoka, njuga hizo zitasikika, naye hatauawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni lazima Haruni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Mwenyezi Mungu, ili asije akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni atavaa kanzu hiyo kutekeleza huduma yake ya ukuhani na sauti yake itasikika wakati anapoingia mahali patakatifu mbele yangu na wakati anapotoka, njuga hizo zitasikika, naye hatauawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka katika mahali patakatifu mbele za BWANA, ili asije akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni lazima Haruni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za bwana, ili asije akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikika hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele za BWANA na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni atavaa kanzu hiyo kutekeleza huduma yake ya ukuhani na sauti yake itasikika wakati anapoingia mahali patakatifu mbele yangu na wakati anapotoka, njuga hizo zitasikika, naye hatauawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Haroni sharti aivae akitumika, milio yake isikilike, akiingia Patakatifu kutokea usoni pa Bwana, hata akitoka, asife.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya BWANA na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni atavaa kanzu ile kwa kutimiza kazi yake ya kuhani na sauti yake itasikilika wakati anapoingia Pahali Patakatifu mbele yangu na wakati anapotoka, kengele hizo zitasikilika, naye hatauawa.