Exodus 28:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni atakivaa kibati hicho kwenye paji la uso wake; kwa hicho kibati atachukua lawama ya makosa ambayo Waisraeli wanaweza kuwa wameyafanya katika kunitolea tambiko takatifu, nami nitazikubali tambiko zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Haruni daima ili zikubalike kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni atakivaa kibati hicho kwenye paji la uso wake; kwa hicho kibati atachukua lawama ya makosa ambayo Waisraeli wanaweza kuwa wameyafanya katika kunitolea tambiko takatifu, nami nitazikubali tambiko zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yo yote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Haruni daima ili zikubalike kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso siku zote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni atakivaa kibati hicho kwenye paji la uso wake; kwa hicho kibati atachukua lawama ya makosa ambayo Waisraeli wanaweza kuwa wameyafanya katika kunitolea tambiko takatifu, nami nitazikubali tambiko zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na kiwe juu ya paji la Haroni, yeye Haroni azichukue manza, wana wa Isiraeli watakazozikora kwa ajili ya vipaji vyao vitakatifu, watakavyomtolea Mungu kuwa vipaji vyao vitakatifu. Na liwe juu ya paji lake siku zote kuwapatia upendeleo machoni pa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni atavaa bamba lile kwenye paji la uso wake. Kwa njia ya bamba lile atabeba mashitaki ya makosa ambayo Waisraeli wanaweza kuwa wamefanya katika kunitolea sadaka takatifu, nami nitakubali sadaka zao.