Exodus 28:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie wamtengenezee vitu vifuatavyo: Kifuko cha kifuani, kizibao, kanzu, joho iliyonakshiwa, kilemba na mshipi. Aroni nduguyo na wanawe watayavaa ili wanitumikie kama makuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kizibau, kanzu, joho lililofumwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Haruni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie wamtengenezee vitu vifuatavyo: kifuko cha kifuani, kizibao, kanzu, joho iliyonakshiwa, kilemba na mshipi. Aroni nduguyo na wanawe watayavaa ili wanitumikie kama makuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Haruni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie wamtengenezee vitu vifuatavyo: Kifuko cha kifuani, kizibao, kanzu, joho iliyonakshiwa, kilemba na mshipi. Aroni nduguyo na wanawe watayavaa ili wanitumikie kama makuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mavazi, watakayomfanyizia, ni haya: kibati cha kifuani na kisibau na kanzu na shati ya nguo ya kunguru na kilemba na mshipi. Haya mavazi matakatifu na wamtengenezee kaka yako Haroni, hata wanawe, wawe watambikaji wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie wamutengenezee vitu hivi: kifuko cha kifua, kizibao, kanzu, na ingine yenye kupambwa vizuri, kofia na mukaba. Ndugu yako Haruni na wana wake watavaa nguo zile kusudi wanitumikie kama vile makuhani.