Exodus 28:43 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni na wanawe watavaa suruali hizo kila wanapoingia katika hema la mkutano, au wanapokaribia kwenye madhabahu, kufanya huduma za makuhani katika mahali patakatifu. Kwa njia hiyo hawataonesha uchi wao na kuwa na hatari ya kuuawa. Hiyo itakuwa kanuni ya kudumu kwa Aroni na wazawa wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Haruni na vizazi vyake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni na wanawe watavaa suruali hizo kila wanapoingia katika hema la mkutano, au wanapokaribia kwenye madhabahu, kufanya huduma za makuhani katika mahali patakatifu. Kwa njia hiyo hawataonesha uchi wao na kuwa na hatari ya kuuawa. Hiyo itakuwa kanuni ya kudumu kwa Aroni na wazawa wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma mahali patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Haruni na vizazi vyake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni na wanawe watavaa suruali hizo kila wanapoingia katika hema la mkutano, au wanapokaribia kwenye madhabahu, kufanya huduma za makuhani katika mahali patakatifu. Kwa njia hiyo hawataonesha uchi wao na kuwa na hatari ya kuuawa. Hiyo itakuwa kanuni ya kudumu kwa Aroni na wazawa wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haroni na wanawe sharti wazivae wakiingia katika Hema la Mkutano au wakiikaribia meza ya kutambikia pale Patakatifu, wasife kwa kukora manza. Maongozi haya yawe ya kale na kale kwake nako kwao wa uzao wake wajao nyuma yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni na wana wake watavaa makapitula hizo kila mara wanapoingia katika hema la mukutano, au wanapokaribia kwenye mazabahu, kufanya kazi za makuhani katika Pahali Patakatifu. Kwa njia hiyo hawataonyesha uchi wao na kuwa na hatari ya kuuawa. Hilo ni sharti la kufuatwa siku zote kwa Haruni na wazao wake.