Exodus 28:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watakitengeneza kizibao cha kuhani kwa nyuzi za dhahabu na sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kukitarizi vizuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tengeneza kizibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watakitengeneza kizibao cha kuhani kwa nyuzi za dhahabu na sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kukitarizi vizuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tengeneza kisibau cha nyuzi za rangi ya dhahabu, za buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa ustadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watakitengeneza kizibao cha kuhani kwa nyuzi za dhahabu na sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kukitarizi vizuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kukitengeneza kisibau na watumie dhahabu na nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na nguo za bafta ngumu, kiwe kazi ya ufundi wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watatengeneza kizibao cha kuhani kwa nyuzi za zahabu na sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kupambwa vizuri.