Exodus 28:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkanda wa kukishikia utatengenezwa kwa vifaa hivyohivyo: Kwa nyuzi za dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa na kuwa kitu kimoja na kizibao hicho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kizibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkanda wa kukishikia utatengenezwa kwa vifaa hivyohivyo: kwa nyuzi za dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa na kuwa kitu kimoja na kizibao hicho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mshipi wa kiunoni uliotengenezwa kwa ustadi ambao ni kitu kimoja na kisibau utatengenezwa kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, za buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, kitani safi iliyosokotwa vizuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mshipi stadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkanda wa kukishikia utatengenezwa kwa vifaa hivyohivyo: Kwa nyuzi za dhahabu, sufu ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa na kuwa kitu kimoja na kizibao hicho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo masombo yake ya kukifunga kifuani pake yawe ya kazi iyo hiyo. Yatengenezwe kwa dhahabu na kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukaba wa kukishikia utatengenezwa kwa vifaa hivyohivyo: kwa nyuzi za zahabu, sufu ya samawi, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa na kuwa kitu kimoja na kizibao kile.