Exodus 29:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu utatwaa mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya maini pamoja na figo mbili na mafuta yake, uviteketeze vyote juu ya madhabahu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, na kipande kirefu cha ini, na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu utatwaa mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya maini pamoja na figo mbili na mafuta yake, uviteketeze vyote juu ya madhabahu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uvichome juu ya madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu utatwaa mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya maini pamoja na figo mbili na mafuta yake, uviteketeze vyote juu ya madhabahu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha yachukue mafuta yote yanayoufunika utumbo na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo yake mawili nayo mafuta yanayoshikamana nayo, uyachome moto hapo mezani pa kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu utatwaa mafuta yote yanayofunika matumbotumbo, sehemu bora ya maini pamoja na figo mbili na mafuta yake, uviteketeze vyote juu ya mazabahu.