Exodus 29:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha utamteketeza kondoo mzima juu ya madhabahu ili kunitolea sadaka ya kuteketezwa; harufu ya sadaka inayotolewa kwa moto itanipendeza mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Bwana; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha utamteketeza kondoo mzima juu ya madhabahu ili kunitolea sadaka ya kuteketezwa; harufu ya sadaka inayotolewa kwa moto itanipendeza mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mteketeze huyo kondoo mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa bwana, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha utamteketeza kondoo mzima juu ya madhabahu ili kunitolea sadaka ya kuteketezwa; harufu ya sadaka inayotolewa kwa moto itanipendeza mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo dume la kondoo wote umchome moto hapo mezani pa kutambikia kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima, ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utamuteketeza kondoo muzima juu ya mazabahu kwa kunitolea sadaka ya kuteketezwa. Harufu ya sadaka inayotolewa kwa moto itanipendeza mimi Yawe.