Exodus 29:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha utachukua mafuta ya huyo kondoo dume: Mkia wake, mafuta yanayofunika matumbo na sehemu bora ya maini, figo zake mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Kondoo huyo ni kondoo wa kuweka wakfu.)
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani, kipande kirefu cha ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha utachukua mafuta ya huyo kondoo dume: mkia wake, mafuta yanayofunika matumbo na sehemu bora ya maini, figo zake mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Kondoo huyo ni kondoo wa kuweka wakfu.)
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwasimika.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo dume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kulia; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha utachukua mafuta ya huyo kondoo dume: Mkia wake, mafuta yanayofunika matumbo na sehemu bora ya maini, figo zake mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Kondoo huyo ni kondoo wa kuweka wakfu.)
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uyachukue mafuta ya huyo dume la kondoo ni mkia na mafuta yaliyoufunika utumbo na kile kipande cha ini na mafigo yake mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo na paja la kuume, maana ni dume la kondoo apasaye siku ya kujazwa gao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utatwaa mafuta ya yule kondoo dume: mukia wake, mafuta yanayofunika matumbotumbo na sehemu bora ya maini, figo zake mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kuume. (Kondoo yule ni kondoo wa utakaso.)