Exodus 29:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo Waisraeli daima watachukua sehemu hizo kutoka katika sadaka zao za amani wanazonitolea mimi Mwenyezi-Mungu na kumpa Aroni na wanawe. Hiyo ni sadaka yao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zote hili litakuwa fungu la milele kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Haruni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa Mwenyezi Mungu kutoka sadaka zao za amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo Waisraeli daima watachukua sehemu hizo kutoka katika sadaka zao za amani wanazonitolea mimi Mwenyezi-Mungu na kumpa Aroni na wanawe. Hiyo ni sadaka yao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Aroni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa BWANA kutoka katika sadaka zao za amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Haruni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa bwana kutoka sadaka zao za amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima siku zote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo Waisraeli daima watachukua sehemu hizo kutoka katika sadaka zao za amani wanazonitolea mimi Mwenyezi-Mungu na kumpa Aroni na wanawe. Hiyo ni sadaka yao kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii na iwe haki yao Haroni na wanawe ya kale na kale kuyapata kwa wana wa Isiraeli, kwani ndio vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa, na viwe vyao, wana wa Isiraeli watakapotoa ng'ombe za tambiko za shukrani, maana vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa ni vyake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo siku zote Waisraeli watatwaa sehemu hizo kutoka katika sadaka zao za amani wanazonitolea mimi Yawe na kumupa Haruni na wana wake. Hiyo ni sadaka yao kwa Yawe.