Exodus 29:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watavila vitu hivyo vilivyotumika kuwaweka wakfu na kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho, lakini mtu mwingine asiruhusiwe kuvila kwani ni vitakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watavila vitu hivyo vilivyotumika kuwaweka wakfu na kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho, lakini mtu mwingine asiruhusiwe kuvila kwani ni vitakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watakula sadaka hizi ambazo kwa hizo upatanisho ulifanywa kwa ajili ya kusimikwa kwao na kuwekwa kwao wakfu. Lakini hakuna mtu mwingine ye yote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watavila vitu hivyo vilivyotumika kuwaweka wakfu na kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho, lakini mtu mwingine asiruhusiwe kuvila kwani ni vitakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na wazile, kwa kuwa ndizo, walizopatiwa upozi nazo, wapate kujazwa magao pamoja na kueuliwa; lakini mgeni hana ruhusa kuzila, kwani ni takatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakula vitu hivyo vilivyotumika kwa utakaso na kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho, lakini mutu mwingine asiruhusiwe kuvikula maana ni vitakatifu.