Exodus 29:42 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sadaka hii ya kuteketezwa itatolewa daima, kizazi hata kizazi, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu, mbele ya mlango wa hema la mkutano ambapo mimi nitakutana nanyi na kuongea nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Mwenyezi Mungu. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Bwana; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sadaka hii ya kuteketezwa itatolewa daima, kizazi hata kizazi, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu, mbele ya mlango wa hema la mkutano ambapo mimi nitakutana nanyi na kuongea nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za BWANA. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za bwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele za BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sadaka hii ya kuteketezwa itatolewa daima, kizazi hata kizazi, mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu, mbele ya mlango wa hema la mkutano ambapo mimi nitakutana nanyi na kuongea nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizi na ziwe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wao wa vizazi vyenu watakazozitoa siku zote mbele ya Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; hapo ndipo, nitakapokutana nanyi, napo ndipo, nitakaposema na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sadaka hii ya kuteketezwa itatolewa siku zote, kizazi kwa kizazi, mbele yangu mimi Yawe, mbele ya mulango wa hema la mukutano ambapo mimi nitakutana nanyi na kuongea nanyi.