Exodus 29:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utawafunga mishipi viunoni na kuwavisha kofia zao. Hivyo ndivyo utakavyowaweka wakfu Aroni na wanawe kuwa makuhani. Hao watakuwa makuhani daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Haruni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Haruni na wanawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utawafunga mishipi viunoni na kuwavisha kofia zao. Hivyo ndivyo utakavyowaweka wakfu Aroni na wanawe kuwa makuhani. Hao watakuwa makuhani daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamsimika Aroni na wanawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Haruni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Haruni na wanawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utawafunga mishipi viunoni na kuwavisha kofia zao. Hivyo ndivyo utakavyowaweka wakfu Aroni na wanawe kuwa makuhani. Hao watakuwa makuhani daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha uwafunge mishipi, yeye Haroni na wanawe, uwafunge vilemba virefu; ndipo, utambikaji utakapokuwa wao kwa hayo maongozi ya kale na kale. Kisha umjaze Haroni gao lake, nao wanawe uwajaze magao yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utawafunga mikaba katika viuno na kuwavalisha kofia zao. Hivi ndivyo utakavyowatakasa Haruni na wana wake kuwa makuhani. Hao watakuwa makuhani siku zote kwa ajili ya sharti la siku zote.