Exodus 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Mose alikuwa anachunga kundi la kondoo la baba mkwe wake, Yethro, kuhani wa Midiani. Mose alilipeleka kundi hilo upande wa magharibi wa jangwa, akaufikia mlima Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Musa alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Mose alikuwa anachunga kundi la kondoo la baba mkwe wake, Yethro, kuhani wa Midiani. Mose alilipeleka kundi hilo upande wa magharibi wa jangwa, akaufikia mlima Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Musa alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Mose alikuwa anachunga kundi la kondoo la baba mkwe wake, Yethro, kuhani wa Midiani. Mose alilipeleka kundi hilo upande wa magharibi wa jangwa, akaufikia mlima Horebu, mlima wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipokuwa akiwachunga mbuzi na kondoo wa mkwewe Yetoro aliyekuwa mtambikaji wa Midiani, akawapitisha mbuzi na kondoo katika hiyo nyika, afike kwenye mlima wa Mungu unaoitwa Horebu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, Musa alikuwa anachunga kundi la kondoo la baba mukwe wake Yetro, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka kundi lile upande wa magaribi wa jangwa, akafika kwenye mulima Horebu, mulima wa Mungu.