Exodus 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyotendewa huku Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘ bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nenda tu, uwakusanye wazee wa Waisiraeli, uwaambie: Bwana, Mungu wa baba zenu, amenitokea, yeye aliye Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo, akaniambia: Nimewakagua ninyi, nikayaona mnayofanyiziwa huku Misri,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenda uwakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia kwamba: Yawe, Mungu wa babu wao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea na kusema: ‘Nimewachunguza ninyi na kuyaona mambo munayotendewa katika inchi ya Misri!